Azania best Quality choice. Good quality wheat is selected after testing it scientifically. The grains are carefully cleaned by modern machines to ensure 100% healthy and clean grains. The cleaned wheat is again grinded in low speed machines by the cold process due to which natural taste, wheaty aroma and nutritional value remain safe and intact.
Usisumbuke kupimiwa Nusu nusu Dukani, Azania imepimwa tayari kuanzia Nusu kilo na kuendelea
Jinsi ya kutengeneza Chocolate Cake kwa kutumia Unga wako bora wa Azania

MAHITAJI
- Unga uliyotayarishwa tayari kwa kupikwa (pakiti moja – 500g)
- Mayai matatu
- Mafuta ya kupikia 80ml
- Maji safi 200ml
- Butter kiasi
Kwa ajili ya topping
- Nunua chokolate yenye karanga
- Maziwa kikombe kimoja
JINSI YA KUPIKA
- Tayarisha oven yako kwa kuiwasha katika moto wa nyuzi 185 centigrade (365F)
- Paka butter kiasi kwenye kikaangio chako kisha kiweke pembeni
- Koroga mayai, changanya na maji safi, mafuta ya kupikia pamoja na unga uliyotayarishwa mpaka vichanganyike vyema
- Nyunyuzia unga wa cocoa au unga wa ngano katika kikaangio chako ulichokipaka butter
- Weka mchanganyiko wa unga, mayai, mafuta ya kupikia pamoja na maji safi ndani ya kikaangio chako kisha ingiza ndani ya oven na funga mlango uache keki iive kwa dakika zitegemeazo aina ya kikaangio chako.
(Iwapo kikaangio chako ni shepu ya mstatili na kina vipimo hivi: 5 X 33 X 22cms = 2 X 13 X 9 inches basi utatumia muda wa dk 40 – 45 kupika keki yako).
(Iwapo kikaangio chako ni shepu ya duara na kina vipimo hivi: 22cms = 9 inches basi utatumia muda wa dk 40 – 45 kupika keki yako).
(Iwapo kikaangio chako ni shepu ya duara na kina vipimo hivi: 15cms = 6 inches basi utatumia muda wa dk 55 – 60 kupika keki yako).
- Tumia toothpick au kijiti cha mbao kisafi kuchomeka katikati ya keki yako kuangalia kama imeiva vyema, baada ya hizo dakika hapo juu kupita. wapo kijiti cha mbao/ toothpick kitatoka bila ya ungaunga basi keki yako imeiva vyema, iepue na uzime jiko. Iwapo kijiti cha mbao/ toothpick kitatoka na unga unga basi ujue bado keki yako haijaiva vyema. Funga mlango na uache iive kwa muda. Hakikisha kijiti kinatoka bila ya unga unga.
- Iache keki yako ipoe kwa dakika 15 – 20 kabla hujaiondoa kwenye kikaangio
Namna ya kutengeneza topping
- Weka sufuria safi kwenye jiko
- Vunja vunja chokolate yako na iweke kwenye sufuria yenye moto
- Ongeza maziwa kikombe kimoja yenye moto
- Koroga mchanganyiko huo mpaka uchanganyike vyema
- Epua mchanganyiko wako weka na anza kupaka kwa kutumia brashi kwenye keki yako ambayo itakua imeshapoa
- Keki yako ipo tayari kwa kuliwa
Waweza kula na soda, chai, juice, maji, maziwa au hata peke yake.
Jinsi ya kupika chapati kwa kutumi unga wako bora wa AZANIA
Mahitaji
- Unga wa ngano (plain flour 1/2 of kilo)
- Siagi (butter vijiko 2 vya chakula)
- Yai (egg 1)
- Chumvi (1/2 ya kijiko cha chai)
- Hiliki (ground cardamon 1/4 ya kijiko cha chai)
- Maji ya uvuguvugu (warm water)
- Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia, kisha tia chumvi na hiliki na uchanganye kwanza, baada ya hapo tia siagi na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee. Baada ya hapo tia tena yai na uchanganye vizuri. Mchanganyiko ukishachanganyika vizuri sasa unaweza kutia maji ya uvuguvugu kidogo, kidogo huku ukiwa unauchanganya ili kupata donge. Baada ya hapo anza kukanda hilo donge mpaka mabuje yote yapotee na unga uwe mlaini, ambapo itakuchukua kama dakika 15. Baada ya hapo tawanyisha unga katika madonge ya wastani (yasiwe makubwa sana au madogo sana) Ukimaliza hapo, andaa kibao cha kusukumia chapati kwa kukitia unga kidogo ili chapati isinatie kwenye kibao. Sukuma donge moja la chapati mpaka liwe flat na kisha weka kijiko kimoja cha mafuta na usambaze. ukisha maliza ikunje (roll). Fanya hivyo kwa madonge yote yaliyobakia.
Baada ya hapo andaa chuma cha kuchomea (fry-pan) katika moto wa wastani. Kisha anza kusukuma chapati (ni vizuri ukaanza na zile ulizozikunja mwanzo ili kuzipa nafasi zile za mwisho ziweze kulainika) ukiwa unasukuma hakikisha zinakuwa flat (na zisiwe nene sana au nyembamba sana) Ukishamaliza hapo tia kwenye chuma cha kuchomea. Acha iive upande mmoja then igeuze upande wa pili. Tia mafuta ama kijiko kimoja kikubwa upande wa chini wa chapati na uanze kuukandamiza kwa juu uku ukiwa unaizungusha. fanya hivyo uku ukiwa unaigeuza kuiangalia kwa chini ili isiungue. ikishakuwa ya brown, geuza upande wa pili na urudie hivyohiyvo mpaka chapati iive. Rudia hii process kwa chapati zote zilizobakia.
Siri ya chapati kuwa laini ni kutia siagi au mafuta ya kutosha kipindi unazikanda na pia kuzikanda mpaka unga uwe laini.
BIDHAA ZA AZANIA NDANI YA SABASABA
BANDA LA AZANIA GROUP LATIA FORA KWA BIDHAA BORA ZA NGANO MAONESHO YA 41 YA BIASHARA YA DAR ES SALAAM
Banda la Azania sabasaba 2017
