e-Mail : info@azaniagroup.company
Call Us : 0710 111 112
Blog

UTAMBULISHO WA AZANIA SPAGHETTI KWENYE SOKO LA TANZANIA

Azania Group of Companies, inapenda kuwajulisha wateja wetu wote kwamba leo  tarehe 30 August 2023, tumezindua bidhaa yetu mpya iitwayo, “Azania spaghetti”. Bidhaa hii inakusudiwa kuleta mapinduzi ya Tambi yenye virutubisho, ladha na uborawa hali ya juu, katika soko la Tambi,Tanzania. 

 Azania Spaghetti inakuja wakati sahihi, ikiwa ni kuitikia ombi na matakwa ya wateja wetu ya muda mrefu, kwa kuja na  bidhaa ya kipekee na bora zaidi yenye kuipa thamani pesa ya walaji.

Azania Spaghetti imetengenezwa kwa umakini mkubwa  kutoka kwenye ngano ya ubora wa hali ya juu ikizingatia viwango vya kimataifa.  Kupitia taarifa hii, Azania Group inatoa wito kwa wateja na wapenzi wote wa tambi kujiandaa kushangazwa na ubora wa Azania Spaghetti, iwe kwa  wapishi wa nyumbani au mfanya biashara ya chakula, Azania Spaghetti inaleta raha katika vinywa vya watumiaji. ilifanyiwa majaribio mbalimbali, ni dhahiri kwamba  bidhaa hii italeta mabadiliko katika soko, lishe bora, na furaha majumbani.

Kuingizwa kwa Azania sphaggeti katika soko la Tanzania, ni mwendelezo wa ukuzi wa uchumi wa nchi yetu kwa  kuongeza ajira kubwa isio ya moja kwa moja kupitia ushirikishwaji vijana wengi katika kusambazaji wa bidhaa hii. Hii ni fursa kwa wafanyabiashara wa juumla na rejareja kuanza kuuza bidhaa hii nchi nzima kuanzia leo tarehe 1 September 2023.

Ikumbukwe kwamba  Azania Group of Companies, ni mojawapo ya makampuni makubwa yanayochnagia ukuaji wa uchumi pamoja na kubadilisha maisha ya maelfu ya watanzania kupitia ajira na kuchochea uanzishwaji wa biashara. 

Endelea kuwa karibu nasi kupitia mitandao yetu ya kijamii, Instagram, Facebook, na Twitter kwa jina la @azaniagroup “

Imetolewa na Azania Group of Companies, Nyerere Rd, Industrial Area