e-Mail : info@azaniagroup.company
Call Us : 0710 111 112

Chocolate Cake kwa kutumia Unga wako bora wa Azania

MAHITAJI

 • Unga uliyotayarishwa tayari kwa kupikwa (pakiti moja – 500g)
 • Mayai matatu
 • Mafuta ya kupikia 80ml
 • Maji safi 200ml
 • Butter kiasi

Kwa ajili ya topping

 • Nunua chokolate yenye karanga
 • Maziwa kikombe kimoja

JINSI YA KUPIKA

 • Tayarisha oven yako kwa kuiwasha katika moto wa nyuzi 185 centigrade (365F)
 • Paka butter kiasi kwenye kikaangio chako kisha kiweke pembeni
 • Koroga mayai, changanya na maji safi, mafuta ya kupikia pamoja na unga uliyotayarishwa mpaka vichanganyike vyema
 • Nyunyuzia unga wa cocoa au unga wa ngano katika kikaangio chako ulichokipaka butter
 • Weka mchanganyiko wa unga, mayai, mafuta ya kupikia pamoja na maji safi ndani ya kikaangio chako kisha ingiza ndani ya oven na funga mlango uache keki iive kwa dakika zitegemeazo aina ya kikaangio chako.

(Iwapo kikaangio chako ni shepu ya mstatili na kina vipimo hivi: 5 X 33 X 22cms = 2 X 13 X 9 inches basi utatumia muda wa dk 40 – 45 kupika keki yako).

(Iwapo kikaangio chako ni shepu ya duara na kina vipimo hivi: 22cms = 9 inches basi utatumia muda wa dk 40 – 45 kupika keki yako).

(Iwapo kikaangio chako ni shepu ya duara na kina vipimo hivi: 15cms = 6 inches basi utatumia muda wa dk 55 – 60 kupika keki yako).

 • Tumia toothpick au kijiti cha mbao kisafi kuchomeka katikati ya keki yako kuangalia kama imeiva vyema, baada ya hizo dakika hapo juu kupita. wapo kijiti cha mbao/ toothpick kitatoka bila ya ungaunga basi keki yako imeiva vyema, iepue na uzime jiko. Iwapo kijiti cha mbao/ toothpick kitatoka na unga unga basi ujue bado keki yako haijaiva vyema. Funga mlango na uache iive kwa muda. Hakikisha kijiti kinatoka bila ya unga unga.
 • Iache keki yako ipoe kwa dakika 15 – 20 kabla hujaiondoa kwenye kikaangio

Namna ya kutengeneza topping

 • Weka sufuria safi kwenye jiko
 • Vunja vunja chokolate yako na iweke kwenye sufuria yenye moto
 • Ongeza maziwa kikombe kimoja yenye moto
 • Koroga mchanganyiko huo mpaka uchanganyike vyema
 • Epua mchanganyiko wako weka na anza kupaka kwa kutumia brashi kwenye keki yako ambayo itakua imeshapoa
 • Keki yako ipo tayari kwa kuliwa

Waweza kula na soda, chai, juice, maji, maziwa au hata peke yake.